Gazeti mmoja la nchini MAREKANI limeripoti kuwa rais BARACK OBAMA wa nchi hiyo amemwandikia barua kiongozi wa IRAN, AYATOLLAH ALI KHAMENEI kujadili uwezekano wa ushirikiano katika kupambana na wanamgambo wa ISLAMIC STATE.
Gazeti hilo limesema OBAMA alituma barua hiyo mwezi uliopita.
Barua hiyo ina kichwa cha habari kinachosema maslahi ya pamoja katika kupamabana na wanamgambo wa ISLAMIC STATE nchini IRAN na SYRIA.
Katika barua hiyo rais OBAMA amesema ushirikianao huo unatarajia
Kukubali kwa IRAN kupunguza kiwango cha mpango wake wa nyuklia.
Wakati huo huo msemaji wa IKULU ya MAREKANI amekanusha taarifa hizo na kusema sera ya nchi hiyo kwa IRAN haijabadilika
COBRA
habari micheo matukio
Idadi ya wanawake
Idadi ya wanawake wanaokwenda hospitali kujifungua imeongezeka Mkoani MBEYA ikilinganishwa na miaka MITATU iliyopita baada ya kuanza kutekelezwa kwa mradi wa matibabu bure kwa wajawazito mkoani huo.
Mganga Msaidizi katika Hospitali ya Rufaa ya MBEYA Kitengo cha Wazazi cha META Dakta GODLOVE MBWANJI amesema hayo mbele ya maafisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya waliofanya ziara ya kushitukiza katika hospitali hiyo kuangalia namna mradi wa matibabu bure kwa wajawazito unavyotekelezwa.
Mradi wa matibabu bure kwa akinamama wajawazito ulianzishwa mwaka 2012 kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Watu wa UJERUMANI na tayari wanawake zaidi ya LAKI MOJA NA ELFU 70 wa Mikoa ya TANGA na MBEYA wamenufaika na huduma hiyo ambapo pia umepunguza vifo vya akinamama wajawazito
Read More;
Mganga Msaidizi katika Hospitali ya Rufaa ya MBEYA Kitengo cha Wazazi cha META Dakta GODLOVE MBWANJI amesema hayo mbele ya maafisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya waliofanya ziara ya kushitukiza katika hospitali hiyo kuangalia namna mradi wa matibabu bure kwa wajawazito unavyotekelezwa.
Mradi wa matibabu bure kwa akinamama wajawazito ulianzishwa mwaka 2012 kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Watu wa UJERUMANI na tayari wanawake zaidi ya LAKI MOJA NA ELFU 70 wa Mikoa ya TANGA na MBEYA wamenufaika na huduma hiyo ambapo pia umepunguza vifo vya akinamama wajawazito
Sekta binafsi zatakiwa kuimarisha viwanda vidogo vidogo
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Masoko ZANZIBAR, RASHID ALI SALIM
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Masoko ZANZIBAR RASHID ALI SALIM amezitaka sekta binafsi kuimarisha viwanda vidogovidogo na viwanda vya kati hasa katika usindikaji wa matunda ili kuwezesha soko la biashara kukua kiuchumi.
Amesema hatua hiyo itawawezesha wafanyabiashara wa sekta binafsi kuzalisha kwa wingi huku wakiendela kupanua soko lao la bidhaa katika ukanda huu wa AFRIKA MASHARIKI ambapo TANZANIA UGANDA , KENYA RWANDA na BURUNDI zimeamua kuingia katika soko la pamoja .
Kauli hiyo ameitoa wakati akifunga semina maalum ya wadau wa sekta binafsi na sekta za umma ambao wamekutana kujadili namna ya utekelezaji wa itifaki ya soko la pamoja ambapo TANZANIA ni miongoni mwa wanachama hao
Serikali ya TANZANIA imekanusha taarifa zilizotoka jana kwenye baadhi ya vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi kuwa maofisa walioambatana na ziara ya Rais wa CHINA SHI NJING PING aliyoifanya mwaka jana waliondoka na idadi kubwa ya pembe za ndovu.
Taarifa hizo zinafuatia ripoti iliyotolewa na taasisi ya kimataifa ya MAREKANI inayojihusisha na uchunguzi wa masuala ya mazingira inayodai kuwa maofisa hao walinunua kiasi kikubwa cha pembe za ndovu.
Akitoa tamko la serikali bungeni mjini DODOMA ,waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa , BERNAD MEMBE amesema taarifa zinazosambazwa katika vyombo vya habari duniani zina lengo la kuichafua TANZANIA na kufifisha harakati zake za kupambana na ujangili na uuzwaji wa pembe hizo duniani.
Biashara ya pembe za tembo ambayo imekuwa ikipigwa vita duniani kote na mataifa mbali mbali kutokana na kutokuwa na tija zaidi ya kuogeza ujangili dhidi ya wanyama hao
Serikali kutunga sheria kali ya kudhibiti dawa za kulevya
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge WILLIAM LUKUVI
Serikali imeliambia Bunge kuwa imetunga Sheria mpya kali zaidi itakayoondoa changamoto zilizokuwa zikijitokeza wakati wa matumizi ya Sheria inayotumika sasa namba 9 ya mwaka 1995 ya Kuzuia biashara haramu ya Dawa za Kulevya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge WILLIAM LUKUVI amesema kuwa Muswada wa Sheria hiyo mpya inayoitwa Sheria mpya ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, 2014 utawasilishwa Bungeni katika Mkutano unaoendelea Bungeni.
LUKUVI, hata hivyo amekiri kuwa Sheria zinazotumika sasa kudhibiti matumizi ya Dawa za Kulevya zinalegalega, jambo linalosababisha kuchukua muda mrefu kuamuliwa kwa Kesi za Dawa hizo.
drake
Drake amekuwa moja ya mastaa ambao wamekuwa wakikaa kwenye headlines mara kwa mara kutokana na sababu mbali mbali.
Safari hii Drake ameangusha kitita
kikubwa cha fedha wakati akiwa anaharakisha kuingia ndani ya club ambapo
waliomuona wanasema jamaa alikuwa kama amekasirishwa na kitu hivi, kwa
hiyo hata huko alikokuwa anaingia huenda hakukuwa na jambo la kheri.
Staa huyo alikuwa anasherehekea birthday
yake wikiendi iliyopita Club Stadium, Washington D.C Marekani ambapo
baadhi ya watu waliokuwa ndani ya club wanasema huenda Drake
alikasirishwa na kitendo cha mmoja ya marafiki zake kupigwa na mtu
asiyefahamika.
Moja ya sababu ambazo huwa zinamuweka
Drake kwenye headlines ni ugomvi, kwa hiyo kama aliingia kushiriki
ugomvi wowote ndani ya club, bado si tukio geni kwa wale wanaomfahamu
staa huyo.
pop
Wakali wa hiphop kutoka Mwanza (88.1 CloudsFM) Young Killer na Fid Q wameingia kwenye headlines na director Nisher ambae ni mshindi kwenye Tuzo za watu 2014 ambapo kinachofanyika ni video ya single ya Young Killer aliyomshirikisha Fid Q.
Unajua Young killer ameiambia millardayo.com mambo yapi matano?
1. Video imetengenezwa ndani ya siku moja tu 2. location ni Tegeta ndani ya sehemu moja tu ambayo ni eneo la kiwanda, 3. Ni single ambayo inazungumzia 13 ambayo ni tarehe ya kuzaliwa Fid Q (August 13) na yeye Young killer aliezaliwa April 13.
4. gharama za video Director mwenyewe amepewa Milioni 4, location imelipiwa shilingi laki 2 ukijumlisha na gharama za magari na pikipiki jumla inafikia kwenye milioni sita na nusu. 5. Pikipiki zilipangwa kutumika lakini zikaachwa, muda uliisha lakini pia Killer alishindwa kuendesha.
picha zote hizi zimetoka kwenye page za instagram za Fid Q >>> HAPA na Nisher >>> HAPA
Unajua Young killer ameiambia millardayo.com mambo yapi matano?
1. Video imetengenezwa ndani ya siku moja tu 2. location ni Tegeta ndani ya sehemu moja tu ambayo ni eneo la kiwanda, 3. Ni single ambayo inazungumzia 13 ambayo ni tarehe ya kuzaliwa Fid Q (August 13) na yeye Young killer aliezaliwa April 13.
4. gharama za video Director mwenyewe amepewa Milioni 4, location imelipiwa shilingi laki 2 ukijumlisha na gharama za magari na pikipiki jumla inafikia kwenye milioni sita na nusu. 5. Pikipiki zilipangwa kutumika lakini zikaachwa, muda uliisha lakini pia Killer alishindwa kuendesha.
picha zote hizi zimetoka kwenye page za instagram za Fid Q >>> HAPA na Nisher >>> HAPA
Stori 7 hot kutoka kwenye magazeti ya leo October 10 2014
Watu saba wameuawa na nyumba zaidi ya 20 kuteketezwa kwa moto katika vurugu zinazodaiwa kuanzishwa na wanakijiji Wilaya ya Kasulu chanzo kikiwa imani za kishirikina ambapo habari zilizothibitishwa na Polisi zinasema vurugu hizo zilitokea juzi usiku na watu waliouawa walikua wakituhumiwa kujihusisha na vitendo hivyo.
Kufuatia hali hiyo watu 18 akiwemo Mwenyekiti wa kijiji aliyeongoza mauaji hayo wanashikiliwa na polisi.
HABARILEO
Sekretarieti ya viongozi wa umma imeamuru Polisi kumkamata mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo na kumfikisha mbele ya baraza la maadili ambapo balozi Jaji mstaafu Hamis Msumi alisema wanao uhakika kiongozi huyo alipokea hati ya kuitwa katika baraza hilo na alitakiwa kufika jana lakini hakutokea.
Alisema atakapofikishwa mbele ya mahakama ataelezwa ni kwa jinsi gani anatuhumiwa na baraza kutumia madaraka aliyonayo vibaya.
MWANANCHI
Wazazi wa mtoto Mazoea mkazi wa Rufiji wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumtupa mtoto huyo kwenye jiko lenye moto wakimtuhumu kuiba shilingi 6000 za jirani yao, Kamanda wa Polisi alisema wazazi hao wanashikiliwa kwa kosa hilo na watapandishwa kizimbani leo kujibu tuhuma hizo.
Kwa mujibu wa ofisa Mtendaji wa kijiji cha Kilimani alisema watuhumiwa hao walifanya kosa hilo baada ya mmoja wa majirani zao kudai ameibiwa kiasi hicho cha fedha ambapo baba yake alimshika miguu na mama yake mikono kisha wakamtupa ndani ya jiko na kuungua vibaya mkono wa kulia wakidai wanamwadhibu kutokana na tabia yake mbaya.
MWANANCHI
Mkazi wa kijiji cha Buriba kata ya Sirari Tarime Buninge Chacha amenusurika kufa baada ya kupigwa mshale kwenye makalio na kuvuja damu nyingi na mtu anayedaiwa kuwa ni mume wake.
Inadaiwa mke wake huyo alikua akipinga binti yao kuozeshwa hali iliyopingwa na mumewe ambae alikasirika na kuamua kumchoma kwa mshale wakati akikimbia kujiokoa, Mwanamke anasema kitendo cha mumewe kumchoma mshale wakati akitetea haki ya mtoto wao kimemfanya aogope kurudi nyumbani kwa madai mumewe anaweza kumuua hivyo ameamua kuishi kwa dada yake.
MTANZANIA
Mahabusu aitwae Andaluswe Mwakapila mkazi wa Olongo Mbeya amejinyonga na kufariki dunia akiwa ndani ya mahabusu katika kituo kidogo cha Polisi Inyala ambapo Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi alithibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema mwili wa marehemu ulikutwa unaning’inia katika dirisha la chumba cha mahabusu.
Alijinyonga kwa kutumia shati lake ambapo chanzo cha kujiua inasemekana kabla ya kufikishwa mahabusu alikua na ugomvi na mkewe ambapo alimpiga kwa kutumia shoka na jembe na kumsababishia majeraha mengi.
MTANZANIA
Jeshi la Polisi Mkoani Njombe linawashikilia wanafunzi 15 wa shule ya Sekondari Njombe kwa tuhuma za kuchoma samani za shule na kufanya vurugu kubwa ambapo Kamanda wa Polisi Njombe Flugence Ngonyani alisema Wanafunzi hao watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.
Alisema wanafunzi hao wanatuhiumiwa kuchoma mali za shule, vifaa mbalimbali vya wanafunzi, kuvunja duka la shule na kuvunja vioo vya nyumba ya mwalimu huku thamani ya mali zote ikitajwa kuwa milioni 113.
UHURU
Serikali inaangalia uwezekano wa kuongeza mbele umri wa kustaafu kwa wenye taaluma kuwa zaidi ya miaka 60 ambapo uamuzi huu wa Serikali unatokana na wenye taaluma wengi kustaafu huku wakiwa bado na uwezo wa kufanya kazi zaidi.
Waziri mkuu Mizengo Pinda alisema jana suala hilo linapaswa kuangaliwa upya na kwa umakini kufuatia kuwepo na changamoto nyingi za upungufu wa wahadhiri katika vyuo vikuu vingi Tanzania.
BREAKING: Uliwahi kusikia kuhusu huyu mtu aliyewaua Wanawake mbalimbali kwa risasi Arusha?
Uliwahi kusikia zile stori za Arusha kwamba Wanawake wanauwawa hovyo kwa risasi wakiwa kwenye magari yao nje ya mageiti ya nyumba na sehemu nyingine? uliwahi kusikia kuhusu wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji hayo? uliwahi kusoma taarifa kwamba ni mauaji mpya yanayochukua kasi Arusha? kama ndio… basi Polisi wametoa taarifa ifuatayo.
Imeripotiwa na Radio One Breaking News inasema >>> ‘ Mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Ramadhan Abdallah Jumanne ambae amekua akiwaua kwa kuwapiga risasi Wanawake mbalimbali jijini Arusha, ameuwawa katika mapambano ya kurushiana risasi na Polisi’
Kaa karibu na AMPLIFAYA ya CloudsFM kuanzia saa moja usiku leo lakini kama utakua mbali na Radio, endelea kuwa karibu na millardayo.com ili nyingine zitakazonifikia nikufikishie.
Subscribe to:
Posts (Atom)



