Drake amekuwa moja ya mastaa ambao wamekuwa wakikaa kwenye headlines mara kwa mara kutokana na sababu mbali mbali.
Safari hii Drake ameangusha kitita
kikubwa cha fedha wakati akiwa anaharakisha kuingia ndani ya club ambapo
waliomuona wanasema jamaa alikuwa kama amekasirishwa na kitu hivi, kwa
hiyo hata huko alikokuwa anaingia huenda hakukuwa na jambo la kheri.
Staa huyo alikuwa anasherehekea birthday
yake wikiendi iliyopita Club Stadium, Washington D.C Marekani ambapo
baadhi ya watu waliokuwa ndani ya club wanasema huenda Drake
alikasirishwa na kitendo cha mmoja ya marafiki zake kupigwa na mtu
asiyefahamika.
Moja ya sababu ambazo huwa zinamuweka
Drake kwenye headlines ni ugomvi, kwa hiyo kama aliingia kushiriki
ugomvi wowote ndani ya club, bado si tukio geni kwa wale wanaomfahamu
staa huyo.