Marekani yakanusha kuandika barua kwa rais wa IRAN

Gazeti mmoja la nchini MAREKANI limeripoti kuwa rais BARACK OBAMA wa nchi hiyo amemwandikia barua kiongozi wa IRAN, AYATOLLAH ALI KHAMENEI kujadili uwezekano wa ushirikiano katika kupambana na wanamgambo wa ISLAMIC STATE.
Gazeti hilo limesema OBAMA alituma barua hiyo mwezi uliopita.

Barua hiyo ina kichwa cha habari kinachosema maslahi ya pamoja katika kupamabana na wanamgambo wa ISLAMIC STATE nchini IRAN na SYRIA.

Katika barua hiyo rais OBAMA amesema ushirikianao huo unatarajia
Kukubali kwa IRAN kupunguza kiwango cha mpango wake wa nyuklia.

Wakati huo huo msemaji wa IKULU ya MAREKANI amekanusha taarifa hizo na kusema sera ya nchi hiyo kwa IRAN haijabadilika