Sekta binafsi zatakiwa kuimarisha viwanda vidogo vidogo
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Masoko ZANZIBAR, RASHID ALI SALIM
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Masoko ZANZIBAR RASHID ALI SALIM amezitaka sekta binafsi kuimarisha viwanda vidogovidogo na viwanda vya kati hasa katika usindikaji wa matunda ili kuwezesha soko la biashara kukua kiuchumi.
Amesema hatua hiyo itawawezesha wafanyabiashara wa sekta binafsi kuzalisha kwa wingi huku wakiendela kupanua soko lao la bidhaa katika ukanda huu wa AFRIKA MASHARIKI ambapo TANZANIA UGANDA , KENYA RWANDA na BURUNDI zimeamua kuingia katika soko la pamoja .
Kauli hiyo ameitoa wakati akifunga semina maalum ya wadau wa sekta binafsi na sekta za umma ambao wamekutana kujadili namna ya utekelezaji wa itifaki ya soko la pamoja ambapo TANZANIA ni miongoni mwa wanachama hao